Supporting information for parents (Swahili)

Boloh: Nambari ya Msaada ya Covid-19 kwa Watu Weusi, Wahindi au familia ya Kabila ya Wachache

Kuhusu Nambari ya Msaada ya Boloh

Nambari ya Msaada ya Boloh ni huduma iliyoanzishwa mnamo Oktoba tarehe 1 na Barnardo kutoka ufadhili wa National Emergencies Trust. Nambari ya Msaada ni mwitikio kwa athari ya janga kwa Watu Weusi, Wahindi au jamii ya kabila ya wachache ambao wameathirika pakubwa.

Wafanyakazi wa Nambari ya Msaada ni Watu Weusi, Wahindi au jamii ya Kabila ya Wachahce, au wako na uzoefu wa awali wa kupeana huduma kwa watoto, vijana wadogo na familia zao kutoka jamii hizi.

Je, tunaweza kusaidia vipi?

Je wewe ni Mtoto Mweusi, Mhindi au mtoto wa Kabila ya Wachache, kijana mdogo, mzazi au mlezi, aliyeathiriwa na Covid-19? Kama ndiyo, labda umepitia hali ya kufiwa, umepata hasara, kukosa ajira, shida za kifedha, una wasiwasi kuhusu kusoma kwa mtoto wako au siku za usoni, una wasiwasi kuhusu rafiki au familia, una masikitiko na wasiwasi kuhusu kufungiwa. Zaidi ya hayo, unaweza kuwa na wasiwasi kuhusu mambo mengine. Unaweza kutuongelesha kuhusu wasiwasi, shida na masikitiko yako kwa wakati huu, na tunaweza kupeana msaada wa kihisia, ushauri halisi na kukutuma kwa mashirika mengine ambayo yanaweza kupeana usaidizi zaidi.

Usaidizi tunaopeana ni wako na wa mtoto (watoto) unaowatunza. Unaweza kutupigia simu au kutuongelesha kupitia kifaa cha mazungumzo mtandaoni kinachopatikana katika tovuti yetu. Huhitaji kushiriki maelezo yako pamoja nasi, lakini kama unataka kuelekezwa kwa timu yetu ya wataalamu wa kimatibabu au huduma nyingine, tutahitaji kuchukua maelezo yako na kushiriki kwa idhini yako. Unaweza pia kufikia ushauri wetu wa tovuti yetu wenye msaada kuhusu mambo tofauti, k.m. ustawi wa kihisia, kusaidia familia, majonzi na hasara.

Je, nini kinafanyika unapowasiliana na nambari ya msaada?

Utapokea jibu kutoka kwa Mshauri wa Nambari ya Msaada mwenye urafiki ambaye atakuongelesha kuhusu jinsi wewe/na/au mtoto (watoto) wako mnapitia. Mshauri wa Nambari ya Msaada atakusikiliza na kukusaidia kufanya uamuzi kuhusu aina ya usaidizi na ushauri unaohitaji. Kwa idhini yako, Mshauri wa Nambari ya Msaada anaweza kukupigia simu nyingi na anaweza kupanga kukupigia tena kwa wakati ambao ni sawa kwako.

Mshauri wa Nambari ya Msaada anaweza kukupangia wewe na/au mtoto (watoto) wako ili kuongea na wataalamu wetu wa matibabu kuwa na vipindi sita vya ushauri na vipindi zaidi zinaweza kupeanwa kama itahitajika. Vipindi vitafanyika kupitia simu mara moja au mara mbili kwa wiki, kulingana na mahitaji na hali ya familia. Kipindi cha kwanza na cha sita kitakuwa cha muda wa dakika 45 kuruhusu tathmini ya awali ya Nambari ya Msaada ili iundwe kwa changamoto tatu kuu ambazo familia au mtu binafsi anapitia, na kipindi cha mwisho ili kujadili na kutambua maendeleo yaliyofanyika wakati wa huduma. Kipindi cha pili hadi cha tano, kila kimoja dakika 30, kitajumuisha usaidizi wa matibabu ya kitaalamu kushughulikia changamoto kuu zilizotambuliwa katika kipindi cha kwanza.

Je, usaidizi unaweza kutolewa katika lugha tofauti?

Washauri wetu wa Nambari ya Msaada wanaweza kutoa huduma katika lugha ya Kiingereza, Kiurdu, Kihindi, Kimirpuri na Kipunjabi. Mnamo Desemba 2020, lugha zinazopatikana zitaongezwa ili kujumuisha Kiamhariki na Kitigrinya na wakalimani wanaweza kutolewa kwa lugha zingine. Vipindi vya kimatibabu vinaweza kutolewa katika lugha zifuatazo: Kiingereza, Kibengali, Kihindi, Kifaransa, Kipunjabi na Kigriki.

Hali Husika

Hali hizi husika zinatoa mifano ya jinsi Nambari ya Msaada ya Boloh inaweza kutoa usaidizi.

Martha ni mama wa vijana wawili ambao wanahudhuria shule ya sekondari ya maeneo. Martha alianza kuwa na wasiwasi kuhusu mtoto wake wa umri wa miaka 15 ambaye alianza kukataa kuenda shuleni kwa sababu aliogopa kuambukizwa virusi vya korona. Martha alijadili hili na mwalimu wa mtoto wake, na yeye akampatia nambari ya Msaada ya Boloh ili kutafuta usaidizi.

Martha aliwasiliana na Nambari ya Msaada na akaongea na Naz ambaye ni Mshauri wa Nambari ya Msaada. Martha alishiriki yafuatayo na Naz: “Mwana wangu alisikia kwamba watu weusi wana uwezekano mkubwa wa kufa kutokana na Covid na sasa anaugua kutokana na mashambulizi ya mahangaiko. Anatuuliza kama tutakufa na hataki kutoka nyumbani kuenda shuleni. Tuna wasiwasi sana kumhusu na hatujui la kufanya.” Baada ya simu kadhaa, Naz alifanya kazi na Martha ili kujadili wasiwasi wake na mahangaiko kuhusu mtoto wake na akakubali mtoto wake apate ushauri na mtaalamu wa matibabu kuongea kuhusu wasiwasi na mahangaiko. Martha na mwana wake wote walianza kupata ushauri wakiwa wametenganishwa, na mtaalamu wa matibabu. Mtoto wa Martha anaendelea kudhibiti mahangaiko yake kuhusu Covid-19.

Hali Husika

Kalhon aliwasiliana na Nambari ya Msaada kupitia mazungumzo mtandaoni baada ya kuona chapisho katika ukurasa wake wa Facebook. Alishiriki kwamba hapo awali aliwekwa kwa likizo halafu akafutwa kazi. Ana wasiwasi kwamba hataweza kulipa kodi ya nyumba na kununua chakula kwa ajili ya familia yake. Wakati wa mazungumzo mtandaoni na Mshauri wa Nambari ya Msaada, alimwambia Mshauri wa Nambari ya Msaada ampigie simu kuongea kuhusu hali yake. Sara, Mshauri wa Nambari ya Msaada, aliwasiliana na Kalhon na wakajadili kuhusu hali yake. Sara alichukua maelezo yote na akakubaliana na idhini ya Kalhon kwamba atafanya upekuzi kiasi na huduma katika Barnardo na mashirika mengine ambayo yanapaswa kusaidia. Sara aliongea na huduma kadhaa za maeneo ambapo Kalhon anaishi na kufanya kazi kutambua huduma kuu mwafaka kusaidia Kalhon na familia yake. Kisha Sara alishiriki maelezo haya na Kalhon ambaye aliwasiliana na hisani ya maeneo ambayo ilimpa yeye na familia yake usaidizi.

 Maono yetu ni kuona watoto Weusi, Wahindi na vijana au watoto wa Kabila ya Wachache wakikuza nguvu ya ndani ili kukabiliana na changamoto za janga na zaidi.  Tungependa sana kufanya kazi nawe kufikia maono haya, kwa hivyo tuongelesha kama unahitaji usaidizi kwa kufanya mawasiliano kupitia:

Simu ya bila malipo: 0800 151 2605

Barua pepe: Boloh.helpline@barnardos.org.uk

Tovuti: https://helpline.barnardos.org.uk/