Boloh - Swahili

Karibu katika Boloh, nambari ya msaada ya COVID-19 ya Barnardo na mazungumzo mtandaoni ya wale wenye umri wa zaidi ya miaka 11

Tupigie simu kupitia 0800 1512605 au tuongeleshe mtandaoni

Je, wewe ni mtoto Mweusi, Mhindi au mtoto wa Kabila ya Wachache, kijana mdogo, mzazi au mlezi, aliyeathiriwa na Covid-19? Unaweza kutuongelesha kuhusu wasiwasi, shida na masikitiko yako wakati huu, na tunaweza kupeana usaidizi wa kihisia, ushauri halisi na kukutuma kwa mashirika mengine ambayo yanaweza kupeana usaidizi zaidi.

Kama wewe ni mtaalamu, unaweza kuwasiliana nasi ili tujadiliane jinsi ya kusaidia mtoto au kijana mdogo anayefanya kazi naye.

Ongea nasi

Tunapatikana kwa mazugumzo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia 1pm-8pm.

Katika lugha nyingi, Boloh inamaanisha ongea.

Kama umeathiriwa na janga na unahitaji ushauri au mtu wa kuongea naye, unaweza kutupigia simu kwa usiri kupitia 0800 1512605 au, kama ungependelea mazungumzo mtandaoni pamoja na mtaalamu mshauri wa usaidizi, unaweza kufanya hivi kupitia mazungumzo mtandaoni ya moja kwa moja kwa kubofya kwenye    aikoni iliyo chini upande wa kulia. Wafanyakazi wetu wenye uzoefu wanasubiri simu zako au mazungumzo mtandaoni Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia 1pm-8pm.

Tuko hapa kukusaidia kama umefiwa, mgonjwa, unahisi ukiwa chini au uko na wasiwasi kuhusu kufungiwa, unahisi umetengwa, una wasiwasi kuhusu marafiki au familia, una wasiwasi kuhusu fedha zako, ukosefu wa ajira, umepitia maonevu au ubaguzi wa rangi, maswala kuhusu ukosefu wa mahali pa kuishi au kuhamishwa, una wasiwasi kuhusu kurudi shuleni/chuo kikuu au suala lolote lingine. Timu yetu ya wataalamu wa akili wanaweza kukupatia usaidizi unaoendelea kwa wakati huu mgumu.

Kupitia simu, washauri wetu wa nambari ya msaada wanaweza kukuzungumzia kwa lugha ya Kiingereza, Kiurdu, Kipunjabi au Kihindi.

Madaktari wetu walio wataalamu wa akili, wanaweza kupeana usaidizi wa kimatibabu kwa lugha ya Kiingereza, Kihindi, Kibengali, Kifaransa na Kipunjabi.